Watanzania watakiwa kutafuta tiba ya Afya ya Akili

0
257

Watanzania wametakiwa kujitokeza kutafuta msaada wa huduma za Afya ya Akili pale wanapoona Kuna changamoto ya Afya ya Akili au kutambua Kuna changamoto ya msongo wa amawazo wajitokeze kwa wataalamu wa huduma hizo ili kuwa na Taifa lenye watu wenye Afya njema ya mwili na akili

Hayo yamesemwa na Kamishna msaidizi ustawi wa Jamii Taifa Baraka Mackona, wakati akifungua semina kwa maafisa ustawi wa jamii, wahudumu wa Afya na azaki zinazotoa huduma za Afya ya jamii Mkoani Arusha iliyoandaliwa na PHEDES Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuhudumia watu wenye matatizo ya Afya ya Akili

Akizungumza na washiriki wa semina hiyo Mackona amesema Serikali imeongeza wigo wa kutoa huduma hizo kuanzia ngazi ya Serikali za mitaa ambako kila Mtanzania anaweza kuhudumiwa kwa urahisi na kutatua changamoto inayomkabili kwenye Afya ya Akili

“Naomba kushauri watanzania watakapojihisi au kujitambua kwamba hali yake ya Afya ya Akili ina changamoto au anakabiliana na changamoto ya msongo wa amawazo ajitokeze kwa sababu sasa hivi tunafundisha wataalamu wengi. Lakini kwa kuanzia wanaweza kuanzia hata ofisi ya mtendaji wa mtaa au kata na Jimbo maana kule tumefikisha kamati zetu na zina mafunzo mazuri ya kuwasaidia Jamii” ameongeza Mackona

Kwa upande wake John Ambrose mkurugenzi wa PHEDES Tanzania ambaye pia ni mkufunzi wa masuala ya Afya ya Akili amesema mafunzo hayo yanatarajia kufanyika kwa awamu mbili kwa lengo la kuwapa elimu watoa huduma za Afya ya Akili ili hasa elimu juu ya janga la UVIKO-19 ambalo liliathili Afya ya Akili kwa Watanzania wengi