Serikali Kuboresha mazingira ya utalii na uwekezaji

0
330

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema baada ya kuzinduliwa filamu ya Tanzania: The Royal Tour hapa Nchini Serikali imejipanga kuimarisha miundombinu ya Utalii ili kukabiliana na idadi kubwa ya wageni wanaokuja kutalii na kuwekeza mara baada kuitangaza Tanzania duniani kote Kupitia filamu hiyo.

Rais Dkt Mwinyi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa filam ya Tanzania: The Royal Tour visiwani Zanzibar ikiwa ni muendelezo wa uzinduzi wa filam hiyo hapa Nchini baada kuzinduliwa Nchini Marekani Aprili 18 mwaka huu.

Akiongea na washiriki wa uzinduzi wa filam hiyo visiwani Zanzibar Dkt Mwinyi ameongeza kuwa tayari dunia imeshajua vivutio na maeneo ya uwekezaji hivyo zinafanyika juhudi za Kuboresha maeneo ya kupokea wageni watakaokuja kuwekeza na kufanya utalii Hapa Nchini

“Zanzibar pekee Kuna hoteli zaidi ya 600 lakini kwa ugeni tunatarajia kupokea wageni kuja kutalii na kuwekeza, inabidi tuangalie namna ya Kuboresha huduma katika Baadhi ya visiwa vyetu ambavyo vitatumika kwa shughuli za kutalii bila kuathili mazingira yake” ameongeza Dkt. Mwinyi

Dkt Mwinyi amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na wazo la kuanzisha filamu ya Tanzania: The Royal Tour ambayo anatarajiwa kutazamwa na watu zaidi ya bilioni Moja ndani ya Mwaka mmoja na kufanya watu wengi kuijua Tanzania hasa Katika Sekta ya utalii na uwekezaji.

“Awali tulikuwa tukijitangaza lakini Nampongeza Sana Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutumia njia ya kuandaa filamu ya Tanzania The Royal Tour ambayo imemfanya kukutana na wafanya Biashara na watu mashuhuri ulimwenguni ambao wameonesha nia ya kuja kuwekeza na kutalii Tanzania” amesisitiza Dkt Mwinyi

Takribani Mwaka mmoja umetumika kufanya maandalizi ya filamu hii na baadae Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa mhusika Mkuu kwenye filamu hii Pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi akishiriki kwenye filamu hiyo yenye lengo la kutanza utalii wa Tanzania.