Ulega ataka matumizi ya teknolojia kuzuia upotevu wa mazao ya uvuvi

0
229

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema sekta ya uvuvi nchini inakabiliwa na changamoto kubwa ya upotevu wa mazao ya samaki hasa dagaa na hivyo kuwataka wadau kutumia teknolojia za kisasa ambazo ni rahisi ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo mkoani Kigoma alipokuwa akizindua maadhimisho ya miaka 10 ya mradi wa Tuungane unaotekelezwa na mashirika ya kimataifa ya Tanzania Nature Conservancy na PathFinder International kwenye vijiji vya kusini mwa mwambao wa ziwa Tanganyika