Parachichi la Tanzania kuuzwa nchini India

0
866

Tanzania kwa mara kwanza imefanikiwa kupeleka kiasi kikubwa cha zao la Parachichi nchini India

Taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini India zinaeleza kupokea Kontena la maparachichi kutoka Tanzania, huku Kontena hilo likiingizwa nchini India kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa wakulima wa zao hilo, wawekezaji waliopo nchini Tanzania na Kampuni ya IG Fruits ya India.

Kontena la maparachichi kutoka Tanzania limewasili nchini India katika Bandari ya Jawaharlal Nehru mjini Mumbai

Balozi wa Tanzania nchini India Anisa Mbega anasema maparachichi hayo yameingizwa nchini India kupitia Kampuni ya IG Fruits ya nchini India kwa kushirikiana na wakulima pamoja na Kampuni ya Avoafrica yenye ofisi zake Makambako Mkoani Iringa itasaidia kufungua fursa nyingi za masoko kwa wakulima wa zao hilo nchini Tanzania