Tuyaendeleze tuliyojifunza kwenye Kwaresma na Ramadhan

0
293

Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka waumini wa Dini ya Kikristo na Kiislam kuendeleza yale yote waliyojifunza wakati wa mfungo wa Kwaresma na Ramadhan ili kuwa na Taifa lenye kuzingatia maadili na tamaduni zinazofundishwa kwenye masomo ya dini hizo

Rais Samia ameyasema hayo wakati wa Baraza la Eid kitaifa lililofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC Jijini Dar es Salaam na kuwataka viongozi wa Dini kuendelea kufundisha maadili mema kwa waumini wao huku akiwataka Wazazi na walezi kuendelea kulea watoto wao Katika misingi ya kidini na Mila za kitanzani

“Kama kutakuwa na malezi mazuri kwa Watoto wetu basi hatutasikia hata haya mambo ya panya road, mwetuaana hawa ni watoto ila inawezekana waliachwa bila kusimamiwa maadili na misingi ya kidini ndio wameingia huko kwenye uharifu” ameongeza Rais Samia akihutubia Baraza la Eid.

Aidha Rais Samia amesema Serikali inaendelea kushughulikia masuala ya itifaki ili kuwasiliana na Mfalme Mohamed (VI) aliyefadhili kujenga msikiti wa kinondoni ili uzinduliwe na kuanza kutumika kama misikiti mingine.

Pia Rais Samia ametumia nafasi hiyo akihutumia Baraza la Eid kuwakumbusha watanzania kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO-19 huku akisema Serikali inakuja na mpango mwingine wa kuhamasisha watu kuchanja maana bado janga hilo bado lipo na inaelezwa kuwa kuna uwezekano wa kuibuka kwa kasi zaidi wa ugonjwa huo hivyo kila Mtanzania anapaswa kuchanja ili kupunguza uwezekano wa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Waislamu ulimwenguni wameendelea kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr mara baada ya kumaliza mfungo wa Ramadhan.