UNFPA kuendelea kushirikiana na wizara ya afya

0
174

Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA) limeahidi kushirikiana na wizara ya Afya ili kuhakikisha huduma bora kwa Mama wajawaziyo zinapatikana

Ahadi hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Naibu Mwakilishi mkazi wa UNFPA Dkt. Wilfred Ochan wakati wa warsha ya Waandishi wa Habari ambapo wamepatiwa ujuzi kuhusu elimu ya Ukunga.

Akitoa ahadi hiyo Dkt. Ochan amesema upatikanaji wa huduma bora kwa Mama wajawazito utapunguza vifo vingi vitokanavyo na uzazi na pia kutasaidia kubaini chanzo cha vifo hivyo.

“Changamoto mpya kwa sasa katika nchi nyingi duniani ni uhaba wa rasirimali ambayo inafanyiwa kazi ili kuondokana na vifo vingi vitokanavyo na uzazi ifikapo 2030, tunatarajia kuyafikia malengo endelevu ya kupunguza vifo chini ya 70 kati ya vizazi hai 100,000.” amesema Dkt. Ochan

Ameongeza kuwa UNFPA inaendelea kushirikiana na wizara ya Afya na Chama cha Wakunga Tanzania, lengo likiwa ni kuhakikisha inawajengea uwezo wa kitaaluma Wakunga katika maeneo mbalimbali nchini

Pia imeboresha huduma za afya zikiwemo wodi za wazazi katika mikoa mbalimbali nchini ambayo ni pamoja na Kigoma, Dodoma, Simiyu na Zanzibar.