Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dokta Mary Mwanjelwa amesema nidhamu na heshima kwa utumishi wa umma kwa sasa imerejea kwa kiwango kikubwa .
Dokta Mwanjelwa amesema hayo katika mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Tbc ambapo amesema kuwa kwa sasa watumishi wengi wa umma wamekuwa na nidhamu jambo ambalo linasaidia katika ofisi nyingi za umma kufikia malengo husika.
Naibu Waziri Mwanjelwa amesema nidhamu imerejea sana katika utumishi wa umma na kuwaomba watumishi wa umma kuendeleza nidhamu hiyo zaidi kwani inajenga taswira nzuri kwa nchi.
Amewataka watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa kufuata misingi iliyowekwa na kuweza kufikia malengo muhimu.
