Tanzania kuomboleza kifo cha Mwai kwa siku mbili

0
333

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza siku mbili za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki, kilichotokea tarehe 21 mwezi hiuu jijini Nairobi.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu imeeleza kuwa, maombolezo hayo yanaanza leo tarehe 29 na kesho tarehe 30.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika kipindi chote cha maombolezo bendera zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania na zile zilizopo kwenye Balozi mbalimbali

Rais Samia Suluhu Hassan amewaomba Watanzania wote kuungana na Wakenya katika kipindi hiki kigumu ambacho wameondokdwa na kiongozi wao.