Mradi wa LNG kuwa chachu ya maendeleo Kusini

0
248

Watanzania wametakiwa kujiandaa kuchangamkia fursa za kibiashara kwenye Mradi wa kusindika Gesi asilia (Liquefied Natural Gas) unaotarajiwa kuanza Mkoani Lindi ambao utazalisha Gesi asilia itakayouzwa ndani na nje ya nchi

Hayo yamesemwa na na mwenyekiti wa Timu ya Serikali ya Majadiliano ya Mradi wa LNG, Charles Sangweni wakati wa kukagua Miradi ya uzalishaji Gesi asilia mnazi Bay na Madimba Mkoani Mtwara wakiwa kwenye Ziara ya kuangalia uzalishaji wa Nishati hiyo inayozalishwa na shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

Sangweni anasema kuwa Mradi wa LNG utafungua fursa nyingi kwa watanzania kwenye Ajira za kidumu na kwa muda huku akiwawasisitiza kujiandaa kwa fani na ujuzi walionao Pamoja na wajasiliamali watakaoona namna ya kujiingizia kipato kwa Biashara ndogo na kubwa Katika eneo la Mradi utakapojengwa na kupita.

Gavana wa Benki Kuu ambaye ni mjumbe wa Timu ya LNG Profesa Florens Luoga amesema ushiriki wa wananchi katika mradi huo utasaidia kulinda mzunguko wa pesa zinazopatikana kutokana na uendeshaji wa Miradi hiyo ndani ya nchi badala ya kuondoka na wageni wanaokuja kufanya Kazi hapa

Kwa upande wake Profesa Sifuni Mchome ambaye ni mjumbe wa Timu ya LNG amesema watanzania wasilale kipindi hiki ni sahihi kuanza kuangalia namna watakavyonufaika na Mradi huo badala kungoja kusukumwa kwenda kuzitafuta fursa zitakazokuwepo wakati wa Utekelezaji wa Miradi huo mkubwa utakaokuwa unasindika Gesi asilia na unaotarajiwa kuzalisha Ajira zaidi ya elfu 40.