Ulinzi waimarishwa kuelekea uzinduzi wa Royal Tour

0
265

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema hali ya ulinzi na usalama mkoani humo ni shwari kuelekea uzinduzi wa filamu ya The Royal Tour.

Kamanda Masejo amesema jeshi la polisi mkoani Arusha limejipanga vizuri kuhakikisha dunia inashuhudia uzinduzi wa filamu hiyo hapo kesho, uzinduzi utakaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).

Ametoa wito kwa Wakazi wa mkoa wa Arusha kuendelea kuwa wakarimu kwa wageni kama ilivyo kawaida yao na kuionesha dunia kuwa Arusha ni kitovu cha utalii.