Naibu Waziri wa Afya akabidhi vyandarua Shinyanga

0
290

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameungana na mwenyeji wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kugawa vyandarua kwa wanawake zaidi ya 400 pamoja na kufikia makundi mbalimbali ya wananchi katika jamii ndani ya Manispaa ya Shinyanga.

Dkt. Mollel ameipongeza Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Amref kutekeleza mkakati huo wa kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuweza kutoa misaada mbalimbali inayogusa maisha ya Watanzania.

Katika Warsha iliyohudhuriwa na wanawake zaidi ya 400, Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuboresha huduma za uzazi, mama na mtoto na kuhakikisha jamii inapata elimu ya kutosha na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

“Asante wakina mama mliokuja hapa kupata elimu ili mkatusaidie kuelimisha wengine na kupunguza vifo vya akina mama na watoto” amepongeza Dkt. Mollel

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel Doris Mollel amesema kuwa lengo la warsha hiyo ni kutoa elimu ya ugonjwa malaria na namna ya kujikinga pamoja na kuhamasisha wanawake kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 ili waweze kujikinga janga hili kubwa la korona, tunaliona linaisha ila bado ugonjwa upo