Emmanuel Macron ashinda Urais Ufaransa

0
178

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameshinda kiti cha urais kwa muhula wa pili, kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini humo na kumshinda mpinzani wake Marine Le Pen.

Katika duru ya pili ya uchaguzi, Macron amepata asilimia 58.54 ya kura huku mpinzani wake Marine Le Pen akipata asilimia 41.46.

Rais Macron anakuwa Rais wa kwanza nchini Ufaransa kuongoza kwa mihula miwili katika historia ya nchi hiyo katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita huku akipongezwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa nchi za Ujerumani, Ubelgiji na Uingereza.

Akielezea matokeo hayo Marine Le Pen amesema anajipanga katika uchaguzi wa Wabunge ambao utafanyika mwezi Juni mwaka huu.