Bunge laahirishwa kufuatia msiba wa Mbunge

0
194

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeahirisha vikao vyake hadi Jumatano wiki hii kufuatia kifo cha Mbunge wa Viiti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa Irene Ndyamkama.

Ndyamkama amefariki dunia jana Jumapili katika hospitali ya Tumbi, Kibaha mkoani Pwani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akitangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma, Spika wa bunge Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa Mbunge Ndyamkama amefarika dunia mara baada ya kuugua ghafla akiwa safarini kuelekea Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu utapelekwa bungeni siku ya Jumatano tarehe 27 mwezi huu kwa ajili ya Wabunge kutoa heshima zao za mwisho, na kwamba mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa mkoani Katavi.