Dkt. Mpango ashiriki uchaguzi

0
119

Makamu wa Rais ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Philip Mpango amewaasa Wakazi wa kijiji cha Kasumo na mkoa wa Kigoma kutumia miradi inayopelekwa katika mkoa huo kujiletea maendeleo.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa mkoa wa Kigoma katika kijiji cha Kasumo wilaya ya Buhigwe mara baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga.

Amesema Serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika mkoa huo ikiwemo ujenzi wa madaraja, barabara na elimu na kuwataka Wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata elimu.

Pia ametumia mkutano huo kuwapongeza Wakazi wa wilaya ya Buhigwe kwa kukubali kutoa eneo la hekari 149.9 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha TEHAMA kinachotarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Songambel.