Matokeo 4 ya ‘Tanzania Royal Tour’

0
1244

Hatimaye Aprili 18, 2022 imewadia siku ambayo Watanzania na dunia kwa ujumla ilikuwa ikiisubiri filamu ya Tanzania Royal Tour yenye lengo la kuitangaza Tanzania na rasilimali zake pande zote za dunia.

Royal Tour ni filamu inayoandaliwa na Mwandishi wa Habari na Mtozi, Peter Greenberg wa Marekani ambayo imewahi pia kufanyika kwa nchi kadhaa ikiwemo Rwanda, ikienda kwa jina la Rwanda Royal Tour.

Zipo faida za kuwepo kwa filamu hii ikiwemo kutangaza utalii wa Tanzania. Vivutio vya Tanzania vingi vinajulikana kwa majina na sifa zake. Filamu hii itasaidia kuwafikisha watalii wengi sana kwenye hatua ya kujua vivutio vingi zaidi ya vile wanavyovijua ikiwemo vivutio ambavyo havijulikani sana kimataifa.

Uwekezaji ni moja ya sekta zitakazonufaika na filamu hii kwani kati ya yaliyomo kwenye filamu hiyo ni sekta mbalimbali zenye fursa za uwekezaji ndani ya Tanzania

Fursa za kibiashara huenda sambamba na uhitaji wa watu wa eneo fulani kwa wakati fulani. kwa kupitia filamu hii iliyosimamiwa vyema na Rais Samia Suluhu Hassan, mataifa jirani na hata ya mbali wanaweza kuvutiwa na kununua bidhaa fulani kutoka Tanzania na hivyo kukuza biashara nchini.

Vilevile ongezeko la watalii litafungua fursa mbalimbali za kibiashara kwa wajasiriamali.

Yote haya yanaenda kwenye kukuza pato la nchi kwani uwekezaji, huku utalii ukiongezeka, uchangiaji wake kwenye pato la Taifa utaongezeka, kadhalika na kwenye uwekezaji.