Serikali kuendelea kukuza ujuzi kwa wanafunzi

0
396

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali kupitia mpango wa 3 wa Taifa wa Maendeleo ya Miaka 5 wa mwaka 2021 hadi 2026 umelenga kukuza Ujuzi wa Watanzania wapatao 681,000

Akisoma hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa, katika Hafla ya ugawaji vyeti na Tuzo kwa Taasisi mbalimbali zilizoonesha Ushirikiano wa kutoa ujuzi wa vitendo kwa Wanafunzi, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema tayari Watanzania Zaidi ya Elfu ishirini na mbili wameshapatiwa ujuzi wa kijiajiri na kuajiriwa.

Kwa Upande wa Uongozi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na mafuzo ya ufundi Stadi (NACTE) wamesema Tanzania bado inahitaji jitihada za ziada kuwekeza katika Ujuzi kwa Wanafunzi ambao wataweza kukudhi Soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Katika hafla hiyo Waajiri Kumi na moja wamepatiwa vyeti na Tuzo mbalimbali kwa kutambua mchango wao wa kuendeleza ujuzi kwa Wanafunzi nchini