Kate Kamba: Msiwe wabishi kuhesabiwa

0
166

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba amewahimiza watanzania kujiandaa na sensa ili kuhesabiwa na kuiwezesha Serikali kuwa na idadi halisi ya watanzania ili kuiwezesha kupanga Bajeti kwa ajili ya kuwaletea maendeleo.

Akizungumza kwenye hafla ya kumpokea makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana, amesema kila mtanzania ana wajibu wa kushiriki kwenye sensa kikamilifu.

Amesema, kusiwepo na watu watakaopuuza zoezi hilo kulingana umuhimu wake huku akiwataka kujitokeza kwa wingi ikiwa ni pamoja na ushiriki wa watu wenye ulemavu.