Watanzania wakumbushwa kulinda umoja na mshikamano

0
302

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria, utawala Bora na Utumishi wa Umma Zanzibar Haroun Ali Suleiman, amesisitiza watanzania kuendeleza umoja na mshikamano ulioasisiwa na viongozi waliopita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Waziri Suleiman ameyasema hayo wakati wa fainali ya mashindano ya 13 ya kuhifadhi Qur’an tukufu yaliyofanyika Dar es Salaam yaliyohusisha vijana wa umri wa chini ya miaka 16 kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika mashariki na Kati.

“Mashindano yameonesha uwezo mkubwa wa vijana wetu walioshiriki mashindano haya na hii ni kutokana na ushirikiano baina ya waandaji na washiriki. Naomba tuzidi kuwekeza kwenye mashindano kama haya ili watoto wetu wazidi kujifunza Zaidi juunya Qur’an na maadili mema”-ameongeza Waziri Suleiman.

Katika hotuba yake Suleiman amekumbusha watanzania kuendelea kujiandaa kushiriki sensa ambayo Ina umuhimu mkubwa wa kujua idadi ya watu na makazi kwa Serikali kujipanga namna ya kutoa huduma muhimu kulingana na mahitaji ya watu.

Fainali ya mashindano hayo yaliyojumuisha washiriki 15 imekamilika kwa mshiriki kutoka Uganda Kateregge Swalahuddin ameibuka mshindi na kujipatia zawadi mbalimbali Pamoja na pesa kiasi cha milioni 11 akifuatiwa na Hamad Suleiman wa Rwanda aliyepata milioni tano nafasi ya tatu ni Ramadhan Nassor kutoka Kenya aliyejipatia Milioni Tatu.