Hamad Rashid : Nyerere alikuwa muumini wa Muungano

0
206

Mwenyekiti wa Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed amesema Mwalimu Nyerere alikuwa muumini mkubwa wa Muungano na hakuwahi kumbagua mtu yoyote kutokana na upande wa Muungano anaotokea.

Akitoa mada kuhusu falsafa ya mwalimu kuhusu Muungano, wakati wa Mdahalo wa Kitaifa unaojadili Miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Baba wa Taifa , Hamad Rashid amesema kuwa wakati wote Nyerere alikuwa akiamini katika usawa wa Muungano.

Ameongeza kuwa Muungano umefika hapo ulipo kutokana na Usimamizi madhubuti wa mwalimu na aliamini katika kuungana na ndio maana alipenda watu wote bila kujali upande wa Muungano anaotokea.