Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili kutoka Nigeria aitwaye Sister Osinachi Nwachukwu maarufu kwa wimbo wake “Ekwueme” amefariki dunia jana jioni katika Hospitali moja iliyoko Abuja nchini Nigeria.
Osinachi alifariki dunia jioni ya jana Ijumaa (April 8, 2022) baada ya Kupambana na ugonjwa usiojulikana kwa takribani miezi miwili huku vyanzo vingine vikidai ni kansa ya koo.
Wimbo wa “Ekwueme” ambao ameshirikiana na Prospa Ochimana unawatazamaji milioni 71 Youtube.
Osinachi ameacha mume na watoto wanne.