Jennifer Lopez achumbiwa tena na Ben Affleck

0
6400

Mwanamuziki wa Marekani Jennifer Lopez (52) na Ben Affeck (49) wamechumbiana tena baada ya kurejesha uhusiano wao mnamo 2021.

JLo alitangaza uchumba huo Ijumaa katika video fupi kupitia jarida la mashabiki wake liitwalo ‘On The JLo.’ Katika video hiyo JLo ameonekana akijikaza kutotokwa na machozi huku akionyesha pete yake ya kijani kibichi, akisema, “Wewe ni mkamilifu“ “You’re Perfect.”

Jennifer alichumbiwa hapo awali 2002 na aligonga vichwa vya habari wakati Ben alipomchumbia kwa almasi ya waridi ya ‘carat’ 6.1 kutoka kwa Harry Winston, lakini Jen alikatisha uchumba huo mapema 2004, na aliolewa na mwimbaji Marc Anthony mnamo Juni mwaka huo huo.

Wawili hao waliishia kuwa marafiki kabla ya kuungana tena kimapenzi na kuwa rasmi kupita Instagram Julai 2021.

Inasemekana “J.Lo yupo mahabani ndindindii na hakika ni vivyo hivyo kwa Ben hasa wakati huu,” chanzo kiliiambia chombo cha ET. “Ben ni mvulana na anafanya mambo yake mwenyewe, ambayo J.Lo anapenda. ana maisha yake mwenyewe na anajulikana kwa njia tofauti na yeye na hajaribu kushindana naye kwa njia yoyote. Wanasaidiana na kupendana tu.”