Butiku: Mwalimu aliwapenda watu wake

0
121

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema, katika maisha yake Mwalimu Nyerere aliweka kipaumbele kwa watu aliowaongoza na aliwatumikia kwa moyo wake wote.

Butiku ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Nyerere amesema, Mwaka 1961 amesema Mwalimu alikataa kuendelea kuwa Waziri Mkuu na kurudi kuimarisha Chama chake cha TANU ambacho ndio kilikuwa karibu na wananchi wakati huo.

Ameongeza kuwa Mwalimu alikuwa mcha Mungu na hakupenda watu waonewe na mara zote alikuwa akisimama kwa ajili ya kuwatumikia watanzania.