Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya ajira nchini

0
301

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu anaeshugulikia kazi, vijana na ajira Patrobas Katambi amesema Serikali itaendelea kufungua na kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta binafsi ili kuongeza fursa na nafasi za ajira kwa watanzania kote nchini

Akizungumza wakati wa kufunga Baraza Kuu la chama cha wafanyakazi katika sekta ya Sayansi na Teknolojia, Elimu ya Juu, Ufundi stadi, Habari, ushauri na Watafiti (RAAWU), Katambi amesema lengo la vyama hivyo si kuleta migogoro sehemu za kazi bali ni kuisaidia serikali na watumishi wakae pamoja.

Aidha Naibu Waziri Katambi amewataka viongozi wa RAAWU kujumuisha katika risala zao majina na vielelezo vya watumishi ambao kwa namna moja au nyingine wamepunjwa stahiki zao na kutopandishwa madaraja licha ya kukidhi vigezo vyote kisheria

Kwa upande wake Mwenyekiti wa RAAWU Taifa Jane Mihanji ameendelea kutoa wito kwa waajiri na serikali kuboresha maslahi ya wafanyakazi nchini ikiwa ni pamoja na kupandisha mishahara yao ili kukidhi hali ya maisha kutokana na wakati tuliopo.