Soko la Karume lawaka moto tena

0
229

Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala Elisa Mugisha amethibitisha kuungua moto soko la Karume kwa mara nyingine baada ya hivi Karibuni kutoka kuteketea kwa moto.

Kwa mujibu wa Kamanda Mugisha tayari Vikosi vya Uokoaji vimeudhibiti Moto huo ambao ulianza katika baadhi ya Vibanda majira ya Saa 11 alfajiri ya leo.

Kamanda huyo wa Jeshi la Zimamoto amesema hasara ambayo inaoneka wazi ni vibanda vyenyewe kuteketea lakini hakuna mali zilizoteketea wala watu waliopoteza maisha