Ukosefu wa Kondomu maeneo ya mialo, chanzo cha ongezeko la VVU

0
266

Hali ya Maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa Mkoa wa Geita imeongezeka kwa asilimia 6.4 na Mwanza imeongezeka hadi kufikia asilimia 7.2, ukilinganisha na hali ya Maambukizi kitaifa ya asilimia 4.7.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI ilipowasilisha ripoti yake Bungeni jijini Dodoma.

Kamati imegundua kuwa ongezeko la maambukizi limetokana na ukosefu wa Elimu kuhusu UKIMWI katika maeneo ya mialo, upatikanaji duni wa kondomu katika maeneo ya mialo na Uhaba wa Rasilimali za kuwasaidia waathirika wa VVU katika maeneo ya uvuvi.

Kamati imeziomba mamlaka zinazohusika kuhakikisha zinatoa Elimu ya UKIMWI katika maeneo hayo na si kusubiri Kamati ya Bunge ndipo watembelee maeneo husika.