Elon Musk amenunua hisa milioni 73.4 (sawa na asilimia 9.2) za mtandao wa Twitter, mamlaka nchini Marekani zimeeleza.
Bilionea huyo mmiliki wa Tesla ametumia TZS trilioni 6.7 kukamilisha ununuzi huo uliofanyika Machi 14 mwaka huu na kumfanya kuwa mmoja wa wamiliki wakubwa wa mtandao huo.
Kwa ununuzi huo, Musk anamiliki hisa mara nne zaidi ya zinazomilikiwa na mwanzilishi wa mtandao huo, Jack Dorsey anayemiliki hisa asilimia 2.25.
Musk ni mtumiaji hai wa Twitter akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 80, lakini hivi karibuni alisema amekuwa akitafakari kuhusu kuanzisha mtandao mpya wa kijamii.