Dkt. Chana: Nipo tayari kufanya Kazi muda wote

0
269

Waziri wa maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana ameahidi kushirikiana na watendaji na watumishi wa wizara yake katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya wizara hiyo.

Ameyasema hayo leo alipowasili katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizopo Mtumba Jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na kuweka bayana kuwa yupo tayari kufanya kazi masaa 24 bila kikwazo chochote.

“Mimi kama Waziri wenu milango ipo wazi saa 24, hakuna wakati sitapatikana iwe usiku, iwe asubuhi hata iwe ni sikukuu na ndio maana ya kuwa mtumishi wa Umma” Ameeleza Dkt Chana

Naye Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa wizara imepata mtu sahihi wa kuitoa ilipo na kuisogeza mbele na kwamba Pindi Chana yupo na timu ya watendaji mahiri na wachapakazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliaasili na Utalii Mary Masanja amemkaribisha Waziri Pindi Chana na kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.