Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba amewaambia wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho kuwa Mgombea wa Urasi wa chama hicho Mwaka 2025 ni Rais wa Sasa Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika Mkutano huo, Makamba amesema, Kwa namna kazi zinavyofanyika mpaka sasa hakuna mwingine wa kushika nafasi ya urais katika uchaguzi ujao zaidi ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Mzee Makamba ameeleza kuwa tayari watanzania wameanza kuonja Asali hivyo ni vyema asali hiyo ikaendelea kulambwa na watanzania na mwenye uwezo wa kuwalambisha watanzania asali hiyo ni Samia Suluhu Hassan pekee.
Makamba amewataka wale wote wanaotamani nafasi hiyo wakae kando na wampishe Rais Samia aendelee kujenga nchi kwa uongozi wake aliofananisha na ubatizo wa maji baridi