Picha: Matukio mbalimbali kutoka Mkutano Mkuu wa CCM

0
186

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma, tayari kuongoza Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ni miongoni mwa mwa makada wa CCM ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho unaofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma.

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa mwa viongozi mashuhuri wa CCM ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho unaofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema na mkewe, Doreen Kimbi wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaoendelea jijini Dodoma.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi kutoka mkoani Iringa, William Lukuvi (kushoto) na Salim Asas, tayari wamewasili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma kunapofanyika mkutano huo.

Waliowahi kuwa Manaibu katibu wakuu wa CCM, Vuai Ali Vuai na Rodrick Mpogolo ni baadhi ya viongozi wastaafu wa CCM waliohudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa Chama hicho unaofanyika hii leo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakiwa wanaburudika na muziki unaoporomoshwa na bendi wa TOT ikiwa ni shamrashamra za wajumbe hao ambao wapo Dodoma kupitisha Mabadiliko ya katiba ya CCM yam waka 2022 na kumpitisha Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania Bara Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Dkt. Bashiru Ally ni miongoni mwa viongozi wastaafu wa CCM ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika hapa mkoani Dodoma hii leo

Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba ni miongoni mwa viongozi wastaafu wa CCM ambao wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika hapa mkoani Dodoma hii leo

Kikundi cha Zanzibar Big Star kutoka Unguja kikitoa burudani kwa baadhi ya wajumbe ambao tayari wapo ukumbini kushiriki mkutano mkuu maalum wa CCM unaofanyika hii leo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) wakiwa katika maandalizi ya kurusha Mbashara matangazo ya mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Mkoani Dodoma.