CCM yamsamehe Membe

0
144

Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana hii leo mkoani Dodoma imemsamehe aliyewahi kuwa waziri wa Mambo ya nje Benard Membe na kumrejeshea uanachama kuanzia hii leo.

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema, msamaha huo ni kwa mujibu wa Ibara ya 48 kifungu cha 8 cha katiba ya CCM na kwamba wamezingatia maombi ya barua zake za kuomba msamaha kwa chama

Alipoulizwa kama ameomba kurudishiwa uanachama, Shaka amesema, Membe amewahi kuandika barua mara tatu kuomba kurejeshewa uanachama wake na sasa NEC imeamua kumrejeshea hadhi hiyo aliyoondolewa tangu mwaka 2018

Mbali na menge NEC pia imemrejeshea uanachama Abdallah Maulid diwani ambaye amewahi kuwa muwakilishi wa jimbo la Jang’ombe ambaye nae aliondolewa hadhi hiyo sambamba na Membe mwaka 2018