Wanafunzi wapewa nafasi kubadili tahasusi zao

0
199

Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2021 wanayo nafasi ya kubadili machaguo ya tahasusi (combination) na kozi mbalimbali wanazohitaji kusoma kulingana na ufaulu wao.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amesema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu kutokujaza fomu (Selfom) kwa uhakika wakati wanachagua combination zau kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao.

“Ofisi ya Rais -TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzi data taarifa zilizo kwenye fomu za mwanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni, hii inatoa nafasi kwa wanafunzi kuweza kufanya mabadiliko ya machaguo yao” amesema Bashungwa

Ameendelea kukufanua kuwa Serikali imetoa fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kubadili machaguo yao ili kutoa nafasi zaidi kwa mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa na utaalam ambao unaendana na machaguo yake hapo baadae.

“Amewataka wazazi kushiriki kikamilifu na kukubaliana na mwanafunzi katika zoezi hili ili pasiwepo na malalamaiko yoyote ya mwanafunzi kuwa amepangiwa machaguo ambayo hakuyachagua hapo baadae,” amesema.