Afya za majeruhi wa ajali Simiyu zaimarika

0
344

Majeruhi nane wa ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Kidulya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Somanda.\

Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji wa Bariadi, Marco Igenge amesema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri.

Katika ajali hiyo, watu saba wamefariki dunia.

Ajali hiyo imetokea baada ya lori lililobeba  tofali kugongana uso kwa uso na l bajaji.

Watu walioshhuhudua ajali hiyo wamesema, ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa lori hilo kujaribu kulipita treka na ndipo lilipokwenda kugongana uso kwa uso na bajaji.