Mwonekano wa watu mashuhuri tuzo za Oscar 2022

0
5080

Picha za baadhi ya watu maarufu katika tuzo za 94 za filamu nchini Marekani (Oscar) mwaka 2022 ,zilizotolewa na Academy of Motion Picture Arts and Science (AMPAS) kwenye Ukumbi wa Dolby Theatre huko Los Angeles.

Mwigizaji Jada Pinkett Simith kavaa gauni kutoka Jean Paul Gaultier X #Glennmartens huku mume wake Will Smith akiwa amevaa suti kutoka kwa Dolce & Gabbana (D&G)

Pia mfanyabiashara Kourtney Kardashian akiwa amevaa gauni jeusi kutoka @tabvintage akiwa ameambatana na Travis Barker ambaye kavaa suti kali kutoka kwa Maison Margiela

Mwigizaji Lupita Nyong’o wa Kenya, kapendeza na gauni lenye nakshi ya ming’ao ya dhahabu kutoka Prada #stylist @micaela

Mwigizaji Tracee Ellis Ross ametokelezea na gauni jekundu ambalo kavalishwa na Carolina Herrera #stylist @karlawelchstylist

Mwigizaji Regina Hall kavaa gauni kahawia mpauko kutoka Vera Wang

Mchezaji wa tenisi Venus Willams kavaa gauni jeupe kutoka @eliesaabworld #stylist @luxurylaw akiwa pamoja na dada yake ambaye pia ni bingwa wa zamani tenisi Serena Willams akiwa amevalia gauni rangi ya waridi kutoka Gucci #stylist @jasonbolden

Mwigizaji na mfanyabiashara Kim Kardashian kavaa gauni kutoka Balenciaga wakati mdogo wake ambaye ni mwanamitindo Kendall Jenner kavaa gauni kutoka Balenciaga pia.

Je ni mwonekano gani umeupenda zaidi ?