Prof. Ngowi afariki dunia

0
236

Profesa Honest Ngowi wa Chuo Kikuu Mzumbe amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea asubuhi ya leo eneo la Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani.

Ajali hiyo pia imesababisha kifo cha dereva wa Profesa Ngowi.

Profesa Ngowi alikuwa safarini kuelekea Kampasi Kuu ya chuo Kikuu Mzumbe iliyopo mkoani Morogoro.