Aliyetoa lugha chafu  kwa Serikali asakwa

0
289

Mahakama nchini Uganda imetoa hati ya kukamatwa kwa mwanaharakati na mtunzi wa vitabu wa nchi hiyo Kakwenza Rukirabashaija, kutokana na tuhuma za kutoa maneno machafu kwa Serikali ya nchi hiyo.
 
Rukirabashaija ambaye amekimbia na kwenda kuishi uhamishoni nchini Ujerumani, anadaiwa kutoa lugha chafu kwa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Serikali yake.
 
Mwanaharakati huyo ambaye alikamatwa mwezi Desemba mwaka 2021 na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi, aliomba ruhusa ya kwenda kutibiwa nchini Ujerumani baada ya kulalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili na maafisa wa usalama nchini Uganda.