PIC yafurahishwa na miradi ya DAWASA

0
292

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji (PIC) imeridhishwa na usimamizi na utekelezaji wa miradi ya Maji ya Kibamba-Kisarawe na Pugu-Gongo la mboto iliyotekelezwa na DAWASA kwa kutumia fedha za ndani.

Akiongea wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye miradi ya maji Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jerry Silaa amesema hali ya usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani inaridhisha hususani katika maeneo yaliyokuwa sugu kama vile Kisarawe na Pugu.

Silaa ameongeza kuwa kwa kasi wanayoenda nayo DAWASA kamati inaamini ifikapo 2025 itakuwa imewafikia Wananchi wote katika eneo lake la kihuduma.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza kuwa kazi kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika, katika usambazaji wa maji ili kuhakikisha yanawafikia wananchi wote.