DPP amfutia mashtaka Abdul Nondo

0
123

Mahakama ya Rufani Tanzania Masjala ya Iringa, imeiondoa kesi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo.

Awali Nondo alikuwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni na kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma huko Mafinga, Iringa.

Kesi hiyo ya Nondo imeondolewa mahakamani baada ya Wakili wa Serikali, Basilius Namkambe kuwasilisha ombi mahakamani hapo mapema hii leo kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na kesi hiyo ambayo ilipelekwa kwa ajili ya kusikilizwa.