Kifua Kikuu bado tatizo nchini

0
117

Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye tatizo kubwa la Kifua Kìkuu.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mwaka 2021 pekee, Tanzania ilikuwa na wagonjwa wa kifua kikuu zaidi ya laki moja na thelathini elfu.

Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya Afya kuelekea maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani hapo kesho Machi 24, ambapo kitaifa yanafanyika mkoani Tanga yakiwa na kauli mbiu inayosema Okoa Maisha, Wekeza katika kutokomeza Kifua Kikuu nchini.

Katika kuadhimisha siku hiyo, wizara ya Afya imewakumbusha Watanania kuwa Kifua kikuu ni ugonjwa unaotibika na kupona kabisa, hivyo hawana budi kuongeza nguvu katika kutambua dalili za ugonjwa huo na kufanya uchunguzi mapema.

Aidha imeihimiza jamii kujitahadhari na mambo yanayochochea kuenea kwa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuepuka misongamano, lishe dubi, unyafuzi kwa watoto na maambukizi ya virusi vya Ukimwi..