Wahamiaji 68 mikononi mwa polisi

0
154

Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji mkoani humo, wamewakamata Wahamiaji 68 wasio na vibali kutoka Ethiopia na Somalia waliokuwa wamejificha katika maeneo tofauti kwenye wilaya za Mwanga na Siha.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Yahaya Mdogo amesema, baadhi ya Wahamiaji hao walihifadhiwa katika kijiji cha Kiberenge wilayani Mwanga.

Wengine wamekamatea wakiwa wanasafirishwa kwa gari eneo la Ngarenairobi wilayani Siha.