Ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa na watu 133 imeanguka katika jimbo la Guangxi nchini China.
Mpaka sasa haijafahamika idadi kamili ya vifo pamoja na majeruhi wa ajali hiyo, na zoezi la uokoaji linaendelea.
Wakati ajali hiyo inatokea ndege hiyo namba MU5735 ilikuwa katika safari zake za kawaida kutoka katika mji wa Kunming kwenda Guangzhou.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema kabla ndege hiyo haijaanguka ilionekana katika eneo hilo kwa takribani saa moja ikizunguka, na moto mkubwa umeonekana eneo ilipoanguka ndege hiyo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.