Askofu Kilaini asherehekea miaka 50 ya utumishi

0
384
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakimkabidhi zawadi Mhashamu Askofu Method Kilaini mara baada ya kushiriki Ibada ya shukrani ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya Upadre wa Askofu Kilaini iliofanyika Kanisa Kuu Katoliki wilayani Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 19 Machi 2022.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Ibada na sherehe ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Methodius Kilaini ambaye ni Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akizungumza na viongozi wa dini, waumini na viongozi wa serikali mara baada ya Ibada ya shukrani ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Method Kilaini iliofanyika Kanisa Kuu Katoliki wilayani Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 19 Machi 2022.

Akizungumza katika Kanisa Kuu Katoliki wilayani Bukoba mkoani Kagera Dkt. Mpango amesema Serikali inatambua na kushukuru mchango wa Baba Askofu Kilaini katika kanisa na jamii ya Watanzania.

Aidha amelipongeza na kulishukuru Kanisa Katoliki kwa kuunga mkono juhudi za Serikali na kwa kutoa mchango mkubwa katika ustawi wa Taifa kiroho, kiuchumi na kijamii kwani limeweza kuifikia jamii hata katika maeneo ambayo Serikali haijaweza kufikisha huduma hususani vijijini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mhashamu Askofu Method Kilaini pamoja na Maaskofu wengine mara baada ya kushiriki Ibada ya shukrani ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya Upadre wa Askofu Kilaini iliofanyika Kanisa Kuu Katoliki wilayani Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 19 Machi 2022.

Dkt. Mpango ameliasa kanisa kufundisha na kulea vijana katika maadili mema na kuthamini kufanya kazi halali kwani nyakati hizi kuna ongezeko la mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii ikiwemo ulevi, vitendo vya rushwa, uvivu, wizi na ufisadi, mauaji ya kutisha na idadi kubwa ya ndoa kuvunjika na kuongezeka kwa watoto wa mitaani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akishiriki Ibada ya shukrani ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Method Kilaini iliofanyika Kanisa Kuu Katoliki wilayani Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 19 Machi 2022.

Kwa upande wake Askofu Method Kilaini ameishukuru serikali kwa ushirikiano iliyompatia kwa kipindi chote cha miaka hamsini ya utumishi wake.

Aidha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mwaka mmoja wa uongozi wake wenye mafanikio makubwa na kazi nzuri aliyoifanya, na kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan taifa limeongozwa kwa utu, amani na mshikamano pamoja na hatua mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.