Geita yajipanga kwa utekelezaji wa mfumo wa Anwani za Makazi

0
323

Naibu Waziri Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew ameonyesha kuridhishwa na mikakati ya mkoa wa Geita ya utekelezaji wa zoezi la mfumo wa Anwani za Makazi ndani ya muda uliopangwa.

Akizungumza katika kikao kazi cha Viongozi na Watendaji kilichoafnyika kwenye ukumbi wa EPZA Mkoani Geita kuhusu operesheni ya utekelezaji mfumo wa Anwani za makazi Mhandisi Kundo amesema, Mkoa wa Geita umejipanga vizuri na ana matumaini kuwa watafanya vizuri katika zoezi hilo.

“Binafsi nimeridhishwa sana na hatua za utekelezaji wa zoezi hili la Anwani za Makazi, kwani mmekuwa wa kweli kwa kuonyesha maeneo yenye changamoto na kuyawekea mikakati imara ya jinsi gani mnakwenda kukabiliana na changamoto hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule amesema, Mkoa wake umejipanga kukamilisha zeozi la utekelezaji mfumo wa anwani za Makazi pindi ifikapo tarehe 15 Aprili, 2022 na kuwa mbele ya muda uliopangwa.