Ajali yaua 22 Morogoro

0
554

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limethibitisha vifo vya watu 22 mpaka sasa, na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha basi la abiria na lori la mizigo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya jioni katika eneo la Malela Kibaoni wilayani Mvomero.

Amesema ajali hiyo imetokea baada ya lori lililokua likitokea Dar es Salaam kwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Congo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ahmeed lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Kamanda Muslim amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki, hivyo kupoteza mwelekeo na kukutana na basi hilo uso kwa uso.

Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro, na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo hiyo.