CHANGAMOTO ZA TANZANIA KWA SASA

0
151

Rais Samia Suluhu Hassan ametaja mambo kadhaa anayoyaona kuwa ni changamoto katika Serikali ya awamu ya sita na anataka ayashughulikie akiwa madarakani.

Rais ameyasema hayo katika mahojiano maalum na TBC, kuangazia mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

ELIMU YA URAIA

“Changamoto yangu ni elimu kwa watu wetu, Watanzania kujifahamu kwamba wao ni Watanzania na kuwa Mtanzania maana yake nini, maana ya elimu ya uraia kwa watu ni elimu ambayo ningependa taasisi zote tushirikiane tuifanye hiyo kazi, kwa kiasi kikubwa kwa watu elimu ya uraia itatusaidia kwenye kuendesha siasa hapa nchini, tutafanya siasa za kistaarabu kila mtu atawajibika kuilinda amani na maendeleo ya Tanzania na utaifa wa Tanzania”

MABADILIKO YA KIUCHUMI YA DUNIA

“Inabidi Tanzania tujitahidi nasi kwenda na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi tuna kila kitu, Tanzania ni kukaa na kuona tunatumiaje vitu tulivyonavyo kuleta maendeleo sio kuvitumia kufaidisha watu wengine sisi tukabaki tunaangalia wanaokuja kushirikiana nasi wapate, na kama nchi tupate”

AJIRA ZA WANANCHI

“Changamoto ni ajira za Wananchi ndio maana tunakazania kuirasimisha sekta isiyo rasmi, tukirasimisha itavutia vijana wengi zaidi kujiajiri na tuibue fursa lakini jiajirini wenyewe.”

KUJIPANGA UPYA KWENYE ARDHI

“Je tunajipangaje kwenye ardhi?, kwa kiasi kikubwa kwa miaka mingi kulikua na upangaji wa ardhi usioridhisha, tunarudije nyuma kurekebisha hayo?, ni changamoto maeneo mengi yameshashikwa, je maendeleo yanayokuja, Wawekezaji tuaowaita tunawapa ardhi ipi?, inabidi tujipange upya kwenye ardhi.“

MITAJI

“Unawaambia vijana wajiajiri, lazima tuwape ardhi, lazima tuwape mitaji, nguvukazi ni wao wenyewe na capital lazima tuwatafutie, na ndio maana tunafanya kazi na mabenki wafungue madirisha washushe riba ili vijana waweze kukopa kwa riba nafuu, tutaweka fedha za kuanzia wakopeshane.”