Waathirika 102 wa biashara ya usafirishaji binadamu warejeshwa

0
1237

Moja ya mafanikio ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita madarakani ni mapambano dhidi ya biashara ya usafirishaji binadamu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amesema katika kipindi hicho Sekretarieti ya wizara hiyo imefanikisha kuwasrejesha waathirika 102 wa biashara hiyo waliopelekwa sehemu mbalimbali na kuwapa hifadhi na huduma za kijamii katika nyumba salama.

Aidha ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja wizara hiyo imefungua kesi nne zinazobusu biashara ya usafirishaji binadamu na kwamba hadi sasa zipo mahakamani.

Kwa mujibu wa Waziri Masauni, wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa mafunzo kwa wadau 280 wanaohusika na utekelezaji wa sheria ya kupinga biashara ya usafirishaji wa binadamu.