Sekta ya habari yaipaisha Tanzania

0
182

Uhusiano mzuri na vyombo vya fedha duniani umewezesha utiaji saini na kuidhinishwa kwa mradi wa Tanzania wa Kidijitali wenye thamani ya dola milioni 150 za kimarekani kutoka katika mkopo wa Benki ya Dunia.

Akielezea mafanikio ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, Waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye amesema Tanzania imeendelea kuungana na dunia kutumia fursa zinazotokea kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo umelenga kuandaa mkakati wa uchumi wa kidijitali pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wa TEHAMA 500 kwenye maeneo ya ubobezi ili kushiriki kwenye uchumi wa kidijitali.

Ameongeza kuwa, mradi huo utafanikisha maboresho ya sheria, na miongozo ili kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya Tanzania ya Kidijitali.

Waziri Nape amesema Tanzania iko tayari kuungana na dunia kutumia fursa zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani.