Viongozi wa dini waomba kushiriki kutoa haki

0
462

Viongozi wa dini nchini wameomba kupewa nafasi ya kushiriki katika vyombo vya utoaji haki, ili kujenga jamii bora kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na Kaimu Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Dkt. Jerald Ndaki wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari kuhusu miikutano iliyofanyika baina ya tume hiyo na wadau mbalimbali katika mikoa mitatu hapa nchini.

” Tumepokea ombi kutoka kwa Viongozi mbalimbali wa dini hapa nchini ambao wameomba kupewa nafasi ya kushirikishwa kwenye vyombo vya utoaji haki, na sisi kama tume tumeona jambo hilo ni sahihi kabisa hivyo tunaangalia ni njia gani sahihi itakayotumika ili kufanikisha jambo hili”. amesema Dkt. Ndaki

Tume ya Utumishi wa Mahakama mpaka sasa imetembelea mikoa ya Tanga, Pwani na Morogoro lengo likiwa ni kupata hali halisi na uelewa wa Wadau ili inapotoa maamuzi yaendane na uhalisia wa eneo.