Naibu Waziri Kundo apita mtaa kwa mtaa kuhamasisha anwani za makazi

0
429

 
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amewataka wakazi wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa  mfumo wa anwani za makazi pamoja na sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu.
 
Mhandisi Kundo ametoa kauli hiyo alipofanya ziara katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Bariadi kwa lengo la kuhamasisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi.
 
Amewataka Wakazi wote wa wilaya ya Bariadi kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mfumo huo ili iwe rahisi kutekeleza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambalo likikamilika litarahisisha ufikishwaji wa huduma pamoja na maendeleo kwa Wananchi.
 
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Posta kutoka wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Caroline Kanuti amewaambia Wakazi hao wa wilaya ya Bariadi kuwa mfumo wa anwani za makazi utarahisisha shughuli za mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo.