Afrika Kusini yaombwa kusuluhisha Russia na Ukraine

0
1392

Rais Cyril Ramaphosawa Afrika Kusini amesema kwamba nchi hiyo imeombwa kuwa msuluhishi wa mgogoro unaoendelea kati ya Russia na Ukraine.

Ramaphosa hajaweka wazi ni nani aliyewasilisha ombi hilo, lakini ameeleza kwamba amezungumza na Rais Vladimir Putin wa Russia na kumsihi kutafuta usuluhishi wa mgogoro huo.

Ameeleza kwamba kutokana na uhusiano wake na Russia na kama mmoja wa wanachama wa BRICS, Afrika Kusini imeombwa kufanya kazi ya usuluhishi.

Nafasi ya Afrika Kusini katika mgogoro huo ilizua mjadala baada ya kutokupiga kura katika azamio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kuishinikiza Russia kusitisha mashambulizi dhidi ya Ukraine.

Ramaphosa amesema Taifa hilo la Kusini mwa Afrika halikupiga kura kwa sababu azimio hilo halikutoa nafasi ya kushirikisha pande zote na amelituhumu baraza hilo kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kuhakikisha kunakuwa na amani na usalama.