Balozi wa Nigeria nchini Dkt. Hamusu Takalmawa ameeleza kufurahishwa na utulivu wa hali ya kisiasa nchini na kusema ni moja ya kichocheo muhimu cha kuvutia Wawekezaji.
Akizungumza na Wafanyakazi wa kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara mara baada ya kutembelea kiwanda hicho Balozi Takalmawa amesema Watanzania hawana budi kujivunia hali ya utulivu wa kisiasa iliyopo kwa kuwa ni nyenzo muhimu ya kujiletea maendeleo.
Amesema uwepo wa rasilimali ya ardhi yenye rutuba unaweza kuwavutia Wawekezaji zaidi kutoka Nigeria, na kuwataka wazawa kujiimarisha zaidi katika sekta ya kilimo.
Naye Meneja Mkuu wa kiwanda hicho cha saruji cha Dangote Mhandisi Normandy Chan amesema kiwanda hicho kilichoajiri zaidi ya Wafanyakazi elfu mbili kinazalisha chini ya uwezo wake kwa asilimia 50 na kwamba jitihada zinafanyika ili kufikia lengo la kuzalisha tani milioni tatu badala ya milioni 1.4 ya sasa